Tuesday, 18 March 2014

OMBWE LIMEJAA


OMBWE LIMEJAA
Na Labaan Shabaan

K
wenye taifa lililokonga
na kugonga nusu karne
Tunashurutika kushangilia
Hata kwenye kinamasi maishani
Tunabidika kusifu mawi yanayotuburuza
Wakati wengine wanadondoa wadudu
Kwenye nyama ili wale
Nyama choma,
Nyama kaanga
Karanga chapo
Kunao wanoteua nyama ya mafuta
Kwenye nyama safi na freshi
Kunao wanaoishi na kunguni
Ilhali wengine wamewaona
Magazetini, vitabuni, majaridani
Kuwasikia pia
Redioni, Runingani  
na  Kwenye masimulizi


M
bona linatujuzu kupendana kwenye vyombo vya usafiri
Madaladala, mabasi, tuk tuk ndege, meli, merikebu, boda boda…
Twaambiwa tukae wanne wanne ama wawili wawili na ndivyo ilivyo
Ni kwenye matatu iliyojaa fondogoo:
Ujaka wa kunyarafisha unukao mff na fee!
Unamsongea na kumsogelea hata aliyetoka jela jana
Twacheka na kuimba ndani ya basi lililobeba
Samaki, dagaa, mbuzi, kondoo waliao mtawalio
Na bado twapendana na kushangiliana mle mle
Wampa mwenzako Sambaza/Kadunga
Aketi sako kwa bako nawe
Hujali hubali
Ama heri punda afe na mzigo ufike?
Haya ndo maisha,
Maisha ya ashurutishwaye
Ili ajiite mwenye nchi
Mwenye nchi mwenye uwezo finyu
Uwezo wa kwenda debeni
Maamuzi mengine waonee runingani.





H
eri mvua izidi kunyesha sasa
Ili kazi yangu ya kuosha bata idumu
Mshahara wangu uzidi mvua ikinya
Bata ajichafue topeni
Na ninakuwa na kazi nyingi ya punda
Ni afueni aisee kwani tutalia wapi?
Mshahara haijambo hapa
Endapo hakunyeshi
Basi bata hachafuki
Na hivyo sina kazi
Swaleh Mdoe u wapi
Uwaambie watafakari hilo!

©December 2013

2 comments: