OMBWE LIMEJAA
Na Labaan Shabaan
K
|
wenye
taifa lililokonga
na
kugonga nusu karne
Tunashurutika
kushangilia
Hata
kwenye kinamasi maishani
Tunabidika
kusifu mawi yanayotuburuza
Wakati
wengine wanadondoa wadudu
Kwenye
nyama ili wale
Nyama
choma,
Nyama
kaanga
Kunao
wanoteua nyama ya mafuta
Kwenye
nyama safi na freshi
Kunao
wanaoishi na kunguni
Ilhali
wengine wamewaona
Magazetini,
vitabuni, majaridani
Kuwasikia
pia
Redioni,
Runingani
na Kwenye masimulizi
M
|
bona
linatujuzu kupendana kwenye vyombo vya usafiri
Madaladala,
mabasi, tuk tuk ndege, meli, merikebu, boda boda…
Twaambiwa
tukae wanne wanne ama wawili wawili na ndivyo ilivyo
Ni
kwenye matatu iliyojaa fondogoo:
Ujaka
wa kunyarafisha unukao mff na fee!
Unamsongea
na kumsogelea hata aliyetoka jela jana
Twacheka
na kuimba ndani ya basi lililobeba
Samaki,
dagaa, mbuzi, kondoo waliao mtawalio
Na
bado twapendana na kushangiliana mle mle
Wampa
mwenzako Sambaza/Kadunga
Aketi
sako kwa bako nawe
Hujali
hubali
Ama
heri punda afe na mzigo ufike?
Haya
ndo maisha,
Maisha
ya ashurutishwaye
Ili
ajiite mwenye nchi
Mwenye
nchi mwenye uwezo finyu
Uwezo
wa kwenda debeni
Maamuzi
mengine waonee runingani.
H
|
eri
mvua izidi kunyesha sasa
Ili
kazi yangu ya kuosha bata idumu
Mshahara
wangu uzidi mvua ikinya
Bata
ajichafue topeni
Ni
afueni aisee kwani tutalia wapi?
Mshahara
haijambo hapa
Endapo
hakunyeshi
Basi
bata hachafuki
Na
hivyo sina kazi
Swaleh
Mdoe u wapi
Uwaambie
watafakari hilo!
©December
2013



Nazifuatilia tena kwa makini kubwa sana mjomba...kazi safi.
ReplyDeleteShukran sana Kaka Lowoi.
ReplyDelete